Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS DKT. SAMIA AWASILI JIJINI LUANDA NCHINI ANGOLA KWA AJILI YA ZIARA YA KISERIKALI YA SIKU 3


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa 4 De Fevereiro Luanda kwa ajili ya Ziara ya Kiserikali ya siku 3 nchini Angola tarehe 07 Aprili, 2025. Rais Dkt. Samia amealikwa na Rais wa Angola Mhe. João Manuel Gonçalves Lourenço na lengo la Ziara hiyo ni kukuza na kuimarisha zaidi mahusiano ya kihistoria na kidugu baina ya Tanzania na Angola.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Mhe. Téte António mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa 4 De Fevereiro Luanda kwa ajili ya Ziara ya Kiserikali ya siku 3 nchini Angola tarehe 07 Aprili, 2025.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com