
Na Hadija Bagasha - Tanga
Jopo la Wataalamu zaidi ya 40 kutoka kwenye taasisi mbalimbali za Kisheria kupitia kliniki ya utatuzi wa msaada wa sheria ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wametua Mkoani Tanga tayari kwa kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi wanaokabiliwa na migogoro mbalimbali ikiwemo ya ardhi kuanzia Aprili 8 mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian ametoa taarifa hiyo Aprili 4,2025 katika mkutano wake na waandishi wa habari wa Mkoa wa Tanga ambapo amesema kliniki hiyo ya msaada wa kisheria ya Rais Samia inatarajiwa kumaliza migogoro mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuwafikishia kwa ukaribu zaidi wananchi huduma hiyo.
Balozi Dkt. Batilda amesema uwepo wa kampeni hiyo katika Mkoa Tanga itasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua migogoro iliyopo ambayo mingine imedumu kwa muda mrefu huku akiwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo na kwamba serikali itatoa ratiba maalumu ya wapi wananchi watatakiwa kwenda kwa ajili ya kukutana na jopo hilo la wataalamu ili kupata ufumbuzi wa migogoro yao huduma ambayo itatolewa bila gharama yeyote.
"Kampeni hii itazinduliwa katika viwanja vya Tangamano siku ya tarehe nane mwezi wa nne ikijumuisha Halmashauri zote za Mkoa wa Tanga na itashuka hadi ngazi ya kata vijiji na mitaa ",amesema Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt. Batilda Burian.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga amesema shabaha ya kampeni hiyo ni kuongeza uelewa wa masula ya kisheria, jamii iweze kutambua masula mazima ya kisheria, hususani haki za wanawake, watoto, wazee, watu wenye ulemavu na makundi yote kwa ujumla wake.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema jambo la pili kwenye kampeni hiyo ni kuimarisha huduma ya ushauri wa kisheria kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia , wengi wakiwa watoto , wakina mama na wakina baba.
Batilda amesema jambo la tatu ni kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu elimu ya sheria kwa uma, masuala ya haki na wajibu pamoja na misingi mizima ya utawala bora, hiku suala la nne likiwa kutoa elimu ya usimamizi wa miradhi na masuala mazima ya urithi wa ardhi , haki ya kumiliki mali.
"Jambo la tano ni utatuzi wa migogoro kwa viongozi wa serikali za mitaa, watendai wa kata , vijiji, wajumbe wa mabaraza ya ardhi kwa kushirikiana na wazee maalumu , machifu, viongozi wa dini na serikali, nipongeze sana timu hii nimeambiwa kwambackambi hii arusha imeweza kutatua mgogoro uliodumu kwa takribani miaka 27,"amesema Mkuu huyo wa Mkoa.
Kwa upande wake mratibu wa kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia Mkoa Tanga ambaye ni Afisa uchunguzi mkuu kutoka Wizara ya Katiba ya Sheria Laurent Burilo amesema kwamba katika maeneo mengi waliyokwisha kuyafikia changamoto kubwa zilizojitokeza ni changamoto za migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ni kilio kwenye maeneo mengi jambo jingine amesema masula ya ndoa na matunzo ya watoto ikiwemo mirathi.
Burilo ametolea mfano Mikoa 23 ambayo wameifikia amesema kwamba wamekumbana na migogoro mingi kwamfano Mikoa 22 ambayo wameifikia wamefanikiwa kuwafikia wananchi zaidi ya milioni 2 na kwamba wamekumbana na migogoro zaidi ya elfu ishirini kati ya migogoro hiyo migogoro zaidi ya 4000 imetatuliwa na kuisha kabisa ambapo wamekumbana na migogoro mingine ambayo imedumu kwa zaidi ya miaka kumi hadi 20.
"Kupitia kampeni hii unakuta mgogoro tunaumalizia ndani ya siku moja au mbili na kuisha kwa hiyo ni rai yetu wananchi wajitokeze ili waweze kupata msaada na migogoro mingine ambayo inahitaji mahakama tunawashauri wananchi kwenda kwenye mahakama, "amesisitiza Burilo.
Social Plugin