Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SIGARA, POMBE ZACHANGIA ONGEZEKO LA WAGONJWA WA MACHO


Na Hadija Bagasha - Tanga

Matumizi ya sigara na pombe yametajwa kuwa ni moja ya sababu zinazopelekea ongezeko la wagonjwa wa macho siku hadi siku.  

Ugonjwa wa macho umetajwa kuwa ni changamoto ambayo imekuwa ikiongezeka ikihusishwa na sababu kadhaa ikiwemo matumizi hayo ya sigara,  pombe na wagonjwa kutumia dawa za macho bila kupata ushauri wa kitaalamu. 

Katika kambi ya siku mbili ya macho ambayo inaendelea katika shule ya sekondari Usagara inayoratibiwa na taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania kwa kushirikiana na Mbunge wa jimbo la Tanga Ummy Mwalimu ambapo idadi ya watu wameonekana kumiminika kwenye huduma hiyo wakihitaji huduma za matibabu. 

Mbunge wa jimbo la Tanga Ummy Mwalimu ametoa wito kwa wananchi kuacha kutumia dawa za macho kiholela bila kupata ushauri wa kidaktari kutokana na sababu za kitaalamu zinazoonyesha sababu hiyo kama ugonjwa wa macho. 

"Ummy amesema kwamba kutokana na uwepo wa changamoto ya macho hasa kwa baadhi ya wananchi katika jimbo hilo ameona ni vyema kuwepo na kambi hiyo ambayo itakuwa mkombozi kwa wananchi ambao wanashindwa kuoata huduma za matibabu kutokana na sababu za kiuchumi. 

"Nitumie fursa hii kutoa wito kwa wananchi kutumia nafasi hiyo kujitokeza kwa wingi ili kufanyiwa uchunguzi na hatimaye kuweza kupata matibabu ya changamoti zitakazobainika, "alisisitiza Mbunge Ummy. 

Kwa upande wake Mratibu wa kambi za macho wa Bilal Muslim Mission of Tanzania Ally Sharif amemshukuru Mbunge huyo kwa kuishawishi kambi hiyo kuja kwa mara ya pili katika Jiji la Tanga kutokana na kuwepo kwa wananchi wenye uhitaji wa huduma za macho.

Mratibu huyo amesema kwamba wanatarajia kuwaona wagonjwa zaidi ya 5000 kwa kuwapatia miwani,  dawa,  na kufanya upasuaji kwa wagonjwa watakaogundulika kuwa na tatizo la mtoto wa jicho. 

"Awali tulipokuja wagonjwa walikuwa ni wengi mno tulitoa matibabu tukaondoka lakini Mbunge wa jimbo la Tanga Ummy Mwalimu alituomba turudi tena na hivyo tukakaona tuje tena kwenye kambi hii na kutoa huduma kwa wananchi hivyo tumpongeze sana kwa namna anavyowajali wananchi wake hasa katika sekta ya afya, "alisema 

Naye Mratibu wa kambi ya macho Mkoa Tanga ambaye ni Daktari Bingwa wa macho katika Hosoitali ya Rufaa ya Mkoa Tanga Bombo Dkt Hussein Tayebji amesema sababu zinazochangia watu kuwa na matatizo ya macho ni kwamba watu hawana utamaduni wa kwenda kupima macho hospitalini mara kwa mara wakati mwingine kutokana na sababu za kiuchumi.

"Lazima watu waje hospitali wapime afya ya macho wajue tatizo lao kama ni dawa matibabu yake ni miwani au ni dawa au kubadilisha mfumo wa maisha lakini tabia ya kuvuta sigara,  unywaji wa Pombe pia huchangia tatizo la macho, "alisema Dkt huyo. 

Baadhi ya wagonjwa waliopatiwa matibabu ya macho katika kambi hiyo wamempongeza Mbunge Ummy kwa kuwajali wanyonge ambao kama sio uwepo wa kambi hiyo wangelazimika kulipia huduma za matibabu katika hospitali mbalimbali. 













Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com